Sunday, December 28, 2014

Tuzo Walizoshinda @VanessaMdee Na @diamondplatnumz Zilizofanyika Nigeria.

vanessa mdee tuzo
Mtangazaji/Msanii Vanessa Mdee na  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wamewakilisha vizuri Tanzania kwa kushinda tuzo zingine kubwa Nigeria za AFRIMA.
Vanessa ameshinda tuzo ya Best Female Artist in East Africa [Msanii bora wa kike Afrika Mashariki ] huku Diamond akishinda Tuzo Ya Best Male Artist in East Africa [ Msanii bora wa kiume Africa Mashariki] . Tuzo ya Diamond ilipokelewa na Peter Msechu ambaye pia alikuwa kwenye kuwania tuzo hizo.
vanessa mdee tuzo 3
peter 2 peter 3

Hongera kwao na Peter Msechu kwa kuwakilisha vizuri.

Ludacris amchumbia girlfriend wake raia wa Gabon kwa ‘style’

Hatimaye rapper Ludacris amemchumbia girlfriend wake wa miaka minne, Eudoxie Fabiola Agnan.
screenshot2014-12-26at110340pm_zps80af3e9c
Kufanya hivyo, rapper huyo alichukua ndege binafsi hadi Costa Rica akiwa na watu wake wa karibu akiwemo binamu yake Monica na mumewe Shannon Brown.
screenshot2014-12-26at111158pm_zps1823b90b
Wakati ndege hiyo ipo juu ya uwanja wa mkubwa, Eudoxie aliangalia chini na kuona maneno: Eudoxie, Will You Marry Me”yaliyokuwa yamechorwa kwenye majani.
Ludacris-girlfriend-Eudoxie-Agnan-pic
Eudoxie alizaliwa nchini Gabon kwenye familia ya kawaida na mama aitwaye Jermaine Agnan. Alihamia Marekani mwaka 2001 akiwa na miaka 15.
Eudoxie-Agnan-Ludacris-girlfriend_image
Eudoxie akiwa na mama yake enzi za utoto

Eudoxie-Agnan-Ludacris-girlfriend_picture

Alicia Keys na Swizz Beatz wapata mtoto wa pili wa kiume

Muimbaji Alicia Keys aliyekuwa mjamzito na mumewe Swizz Beatz wamepata mtoto wa pili aliyezaliwa Jumamosi Dec 27.
alicia_husband
Wanandoa hao wametangaza kupitia Instagram kuwa mtoto wao wa pili aliyezaliwa ni wa kiume na wamempa jina la Genesis Ali Dean.

Keyz na Beatz walifunga ndoa mwaka 2010 na kufanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume aitwaye Egypt miezi miwili baada ya ndoa.

Exclusive New Audio Mkubwa Na Wanawe|Tulia|DOWNLOAD






Saturday, December 27, 2014

Kanye West ana wivu na mafanikio ya Taylor Swift

Ni miaka sita tangu Kanye West ampokonye microphone Taylor Swift alipokuwa akipokea tuzo ya Best Female Video kwenye MTV Video Music Awards lakini bado hakumbali.
Kanye-West
Imedaiwa kuwa Kanye haelewi inakuaje Taylor amekuwa na mafanikio makubwa hadi leo na hiyo inamsumbua kiasi cha kumpa hasira nyingi.
Yeezy anadaiwa kuchukia baada ya kubaini kuwa video ya wimbo wa Taylor ‘Shake It Off’ imeangaliwa mara nane zaidi kwenye YouTube kuzidi yake ya ‘Bound 2′.

Kanye anadaiwa kuchukia zaidi baada ya kubaini kuwa Jay Z amekataa kumhusisha kwenye mipango yake ya muziki na Taylor, Beyonce wala Justin Timberlake.

Madee atoa sababu ya kubadili ratiba ya ujio mpya wa Dogo Janja

Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Madee ambaye aliwaahidi mashabiki wa kundi hilo kuwa Dogo Janja ataachia wimbo hivi karibuni, amedai ameahirisha mpango huo kutokana na kuingiliana kwa ratiba nyingine.
Madee na Chege akiwa kwenye pozi
Akizungumza na Junior kaguo leo, Madee amesema imelazimika Dogo Janja asubiri kwakuwa kuna wimbo aliofanya akiwa na Chege na Temba Afrika Kusini unayohitajika kutoka mapema zaidi.

“Kuna mabadiliko kidogo ambayo yameingiliana,” amesema rapper huyo. “Kuhusu Dogo janja bado kidogo yupo ningependa kuzungumzia ratiba inayofuata ya Madee, kwa sababu kuna project ambayo tulienda kufanya South Africa kule inatakiwa itoke mapema Januari kwahiyo hicho ndo kitu ambacho kinaangaliwa sana. Then Dogo Janja atakuja pamoja na Raymond. Kwahiy mwakani itatangulia kwanza nyimbo ya Madee na baada ya hapo ndo Dogo Janja atakuja.”

Show Ya Diamond Platnumz Na Mzee Yusuf DarLive












posted by nsajigwa  kapange  bonyeza HAPA kunifollow on twitter

Hii video mpya ya Msami ‘Shake Shake

New Audio Toofan OROBO|DOWNLOAD



Picha,Cristiano Ronaldo Azindua Sanamu Lake huko Ureno

Cristiano Ronaldo ameizindua sanamu yake ya heshima aliyojengewa huko Medeira Ureno juzi , hii imekuja siku moja baada ya mchezaji pekee duniani kuweza kushinda makombe yote kwa ngazi ya klabu katika vilabu viwili tofauti.



Monday, December 22, 2014

Zamwizi 40

Eti kunahajagani yakupeleka mwizikituoni nakesho unakutananae mtaani  hapana minainanjia rahisi ni?

Hakuna tofauti kati mfugaji namkulima


Mambohaya yameaza lini nanikwann hiliswala linachiwa liendelee?

Sunday, December 21, 2014