Saturday, December 27, 2014

Kanye West ana wivu na mafanikio ya Taylor Swift

Ni miaka sita tangu Kanye West ampokonye microphone Taylor Swift alipokuwa akipokea tuzo ya Best Female Video kwenye MTV Video Music Awards lakini bado hakumbali.
Kanye-West
Imedaiwa kuwa Kanye haelewi inakuaje Taylor amekuwa na mafanikio makubwa hadi leo na hiyo inamsumbua kiasi cha kumpa hasira nyingi.
Yeezy anadaiwa kuchukia baada ya kubaini kuwa video ya wimbo wa Taylor ‘Shake It Off’ imeangaliwa mara nane zaidi kwenye YouTube kuzidi yake ya ‘Bound 2′.

Kanye anadaiwa kuchukia zaidi baada ya kubaini kuwa Jay Z amekataa kumhusisha kwenye mipango yake ya muziki na Taylor, Beyonce wala Justin Timberlake.

No comments:

Post a Comment