
Akizungumza na Junior kaguo leo, Madee amesema imelazimika Dogo Janja asubiri kwakuwa kuna wimbo aliofanya akiwa na Chege na Temba Afrika Kusini unayohitajika kutoka mapema zaidi.
“Kuna mabadiliko kidogo ambayo yameingiliana,” amesema rapper huyo. “Kuhusu Dogo janja bado kidogo yupo ningependa kuzungumzia ratiba inayofuata ya Madee, kwa sababu kuna project ambayo tulienda kufanya South Africa kule inatakiwa itoke mapema Januari kwahiyo hicho ndo kitu ambacho kinaangaliwa sana. Then Dogo Janja atakuja pamoja na Raymond. Kwahiy mwakani itatangulia kwanza nyimbo ya Madee na baada ya hapo ndo Dogo Janja atakuja.”
No comments:
Post a Comment